Y

YouLibs

Remove Touch Overlay

Salama Na TOGOLANI SE6 EP09 |CIVIL SERVANT PART 2|SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Duration: 22:08Views: 7.8KLikes: 91Date Created: Mar, 2022

Channel: YahStoneTown

Category: Entertainment

Tags: marcochalimwanafasalamajabirgigy moneymxcartergigi moneysalamanaayyah stonetown yahstonetownjokatekhadijakopadiamondplatnumzfidq

Description: #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460 Kwangu mgeni wetu wa wiki hii ni kioo kwangu, yaani mfano wa kuigwa na mtu anayefaa kutupia wa jicho mara kwa mara pale unapotaka kujivunza mawili matatu kuhusu elimu, maisha, kazi na hata jinsi ya kujibeba. Akiwa kwenye miaka yake ya mwanzo ya Arobaini, Togolani Edriss Mavura ni mtu haswa, aliyepikwa (aliyejipika) akapikika. Kila mtu na KARAMA yake, KADRI yake na KUDRA yake, huu usemi uko kwenye BIO ya account yake ya Twitter ambao una wafuasi zaidi ya lakini mbili (nami nikiwa mmoja wao) ambao kila asubuhi hungoja kwa hamu kutaka kujua Bwana Togolani ataamka na maneno yepi ambayo yatakufanya uyawaze huku siku ikienda, kama ni ya kukufunza au kukufanya uwaze au hata ucheke, hiyo yote itategemea na yeye kaamka vipi. Nilimuuliza kama ni kitu ambacho huwa anakipangilia kabisa pengine siku kabla, pengine kabla hajalala na kama hutumia nguvu nyingi ili pengine asituangushe ‘mashabiki’ zake? Akasema maneno huja tu na huyaweka kwenye draft na muda wa kupostiwa ukifika hufanya hivyo, na pia kaniambia mwanzo ilimshangaza kiasi baada ya kuona asipo post watu humuandikia kumuuliza kama kaamka na kama kila kitu kiko poa. Nadhani hiyo inatosha kukuelezea mwenzetu ni mtu mwenye karama ya kiasi gani. Amezaliwa kwenye familia ya Baba mtumishi wa serikali na Mama ambaye alikua akimpa favors zaidi kuliko Mzee wake, ambaye kwa mujibu wa Togolani, yeye alikua anataka ASOME, ili AMALIZANE NAYE, chochote ambacho alikua anataka kinachohusu elimu Mzee Mavura alikua hana neno kabisa. Na alikua mkali pale alipokua anaona kijana wake hafanyi vizuri shuleni, kidedea kilishikwa mpaka alipoona kijana kaiva then akaacha boti iende yenyewe tu maana bahari ilikua shwari. Wa kiume pekee kwao, ndo maana yeye na Mama yake ni marafiki sana. Sasa ameoa na ana mtoto/watoto (hii topic ilikua haituhusu, maana yeye ni mtu ambaye hataki familia yake iwe kwenye spotlight). Ila ndio ni Baba na muwe ambaye ana enjoy jukumu hilo pia. Pia nilimuuliza kitu gani kilimfanya asomee hiki anachokifanyia kazi, na huwezi kuamini, ambacho anafanya sasa haikuwahi kuwa chaguo lake la kwanza wala, kwanza zamani kabisa yeye alitaka kuwa dereva tu lol, ila alivyokua anakua akataka sana kuwa Wakili, ila kwa jinsi mambo yalivyo sasa, tuseme haikua KUDRA yake. Mengi yameguswa humu, kama kawaida nisingependa kunyofoa sana ili nawe upate kuyaskia au kuyaona mwenyewe yaliyojiri kwa KADRI yako. Tafadhali Enjoy, maana mimi ninajivunia nafashi hii adhimu ya kukaa na Togolani na kusikiliza mitihani na khadithi ya maisha yake, kwa kiasi ambacho tuliweza kupata muda wa kuyazungumza hayo. Hongera kwake kwa kuchagulia na Mama Samia kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea ya Kasini. Mimi na wenzangu tunamtakia Kheri nyingi. Love, Salama. Support us through anchor.fm/yahstonetown/support SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬ ‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬ GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack ‪YouTube Link bit.ly/YoutubeSalamaNa Soundtrack Yeah by @MarcoChali youtube.com/watch?v=Cue1HB4fnLQ Follow: Twitter: twitter.com/YahStoneTown Instagram: Instagram.com/YahStoneTown Facebook: facebook.com/YahStoneTown Channel Administered by Slide Digital Instagram: instagram.com/slidedigitaltz

Swipe Gestures On Overlay